Naibu Waziri wa Madini Dkt. Stephen Kiruswa amesema Sekta ya madini ni nguzo ya maendeleo duniani kote na imesaidia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa taifa na maendeleo ya mtu mmoja mmoja nchini.
Dkt. Kiruso ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wachimbaji Madini na Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania – FEMATA, uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jijini Mwanza.
Amesema katika jitihada za kuikuza sekta ya wachimbaji wadogo, Serikali imetenga jumla ya maeneo nane yenye ukubwa wa kilomita za mraba 112.29 kwenye mikoa ya Mwanza, Geita, Pwani na Shinyanga na kusema Wizara ya madini itaendelea kusimamia sekta hiyo kwa weledi ili malengo ya Serikali yafikiwe.
Naye Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania – FEMATA. John Bina amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha anaisimamia vyema sekta ya madini, ili iweze kuketa tija kwa uchumi wa nchi, wachimbaji na watanzania kwa ujumla.