Mahakama ya Mwanzo ya Ukonga jijini Dar es salaam imemuamuru Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga kutoa kiasi cha Shil. 250,000 kila mwezi kwa ajili ya matumizi ya mtoto.

Mahakama hiyo pia imekataa ombi la DC Odunga la kumtaliki mkewe, Ruth Osoro aliyefunga naye ndoa Serikalini Februari 21, 2010 na kupata cheti cha ndoa B no 0979341.

Katika kesi hiyo, Odunga ambaye ni mdai alitoa ushahidi mwenyewe huku mkewe akitoa ushahidi wake na mashahidi wawili akiwepo dada yake na mke mwenza wa ndoa ya Kikristo.

Aidha, Odunga alilalamikiwa na mkewe Ruth kwa kutokutoa matunzo ya mtoto wao wa kiume (4) kwa kipindi cha miaka mitatu.

Licha ya malalamiko hayo Ruth aliiomba Mahakama isivunje ndoa yake kwa kuwa bado anampenda mume wake huku Odunga akitaka ndoa ivunjwe na apewe ridhaa ya kumlea mtoto huyo.

Benki ya Dunia yaahidi kuineemesha Tanzania
Tarehe ya Uchaguzi Serikali za Mitaa yawekwa hadharani