Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema ameziita taasisi mbili za EWURA na NEMC kutoa taarifa juu ya ukaribu na wingi wa vituo vya mafuta katika maeneo mengi nchini.
Makamba ameyasema hayo hii leo Oktoba 21, 2022 na kusema taasisi hizo zinatakiwa kuwasilisha uchambuzi wa kikanuni za umbali kati ya kituo kimoja cha mafuta na kingine.
Amesema, “Hili jambo tumeliona na uzuri ni kwamba EWURA na NEMC ni Taasisi mbili ambazo zinahusika na mahala ambapo kituo cha mafuta kinatakiwa kiwe na ni umbali ganiuwepo kati ya kituo na kituo naona vituo vya mafuta vimekuwa vingi na wakinipatia taarifa nitaiweka hadharani.”
Katika hatua nyingine, Waziri Makamba amesema kupitia ziara alizozifanya katika mikoa 10 hasa maeneo ya Vijijini aligundua mambo mbalimbali ikiwemo wananchi kutaka umeme uwafikie na ukosefu wa huduma ya mafuta ya kuendeshea vyombo vya moto.