Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amekanusha taarifa zilizoripotiwa na baadhi ya vyimbo vya habari kuwa amepinga zoezi la ‘utumbuaji majipu’.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha hivi karibuni, alipokuwa akisisitiza kuhusu uhamishaji wa mifugo kutoka katika hifadhi ya taifa, Mama Samia ameeleza kuwa yeye aliwataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kufuata taratibu za utumishi wa umma kabla ya kuwawajibisha watumishi wa umma.

Aliongeza kuwa Rais John Magufuli ndiye mwenye mamlaka kisheria ya kuteua, kutengua na kuajiri.

“Rais pekee ndiye mwenye mamlaka ya kuteua, kutengua na kuajiri lakini sijapinga utumbuaji majipu, bali nasisitiza kila mkuu wa mkoa na DC (mkuu wa wilaya) afuate sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma,” alisema Makamu wa Rais.

'Kamanda' Nzowa asimulia alivyokwepa kuuawa na Wauza ‘Unga’
Magufuli atishia kuwatumbua jipu mawaziri wawili walioanza na JK