Shikisho la Mpira wa Miguu Tanzania leo limesaini mkata mpya wa miaka mitatu na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kwa ajili ya udhamini wa ligi kuu Tanzania bara ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni.

Mkataba mpya

Mkurugenzi wa mawasiliano na masoko wa Vodacom Kelvin Twise amesema, mkataba huo unaongezeko la asilimia 40 kutoka kwenye udhamini wa miaka iliyopita ambapo udhamini ulikuwa ni shilingi bilioni 1.6 na mkataba wa sasa utagharimu shilingi bilioni 2.3.

Mkata mpya 5

Twisa amesema ongezeko kubwa la udhamini limekwenda kaktika usafiri wa timu kwasababu timu nyingi zimekuwa zikilalamika kuwa zinapata wakati mgumu kwenye gharama za usafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Kwahiyo katika fedha hiyo ya udhamini, shilingi bilioni 1.2 zitakwenda kwenye timu zote 16, waamuzi wanagharimu zaidi ya milioni 360, maafisa wengine wa mechi ambao wanakuwa nje ya uwanja wao gharama yao ni zaidi ya milioni 62, TFF wao wanapata milioni 183, zawadi kwa ujumla ni milioni 174.

Mkata mpya 2

Akaongeza kuwa hawajaongeza kiasi chochote kwenye zawadi kwasababu waliangalia kati ya kuongeza zawadi au kuzisaidia timu nyingine mpya na zile zenye uwezo mdogo kifedha ili ziweze kupambana kwenye ligi, wakaona ni bora kuongeza kiasi ambacho timu zinapata ili kujiendesha kuliko kuongeza zawadi.

Zaidi ya hapo wataendelea kutoa tuzo ya mchezaji bora wa kila mwezi kama kawaida ambapo imetengwa milioni 18, mchezji bora wa ligi, mwamuzi bora, na kocha bora zenyewe zimebaki kama zamani.

Kwa maana hiyo, ongezeko limekwenda sehemu tatu, kwanza kwenye timu, waamuzi na match officials.

Mkata mpya 5

Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi akafafanua kuhusu mkataba huo jinsi unavyoiruhusu TFF kutafuta wadhamini wengine wa ziada kwenye ligi kuu ambayo inadhaminiwa na Vodacom ilimradi yasiwe makampuni yanayoshindana na mdamini mkuu wa sasa (Vodacom) katika biashara na akaongeza kuwa, mpaka sasa kwa kushirikiana na Vodacom tayari wameshaanza kutafuta makampuni mengine.

Katika hatua nyingine, Malinzi amesema TFF inapambana na rushwa kwasababu inachangia kwa kiasi kikubwa kushusha soka la Tanzania ambapo iliifananisha rushwa na‘ngono’ kutokana na kufanyika kwa usiri mkubwa lakini akawaomba wadau wa soka wasaidiane na TFF ili kuweza kuwabaini watoaji na wapokeaji rushwa wanaoliharibu soka la Tanzania.

TRA Kuendesha Semina Ya Kodi
Valbuena Akubali Kurejea Nyumbani