Mabeste na Lisa wamekuwa stori kubwa sana katika mitandao mbalimbali ya kijamii mara baada ya Lisa kuamua kufunguka kilichopelekea ndoa yao kuvunjika kisa alichotaja kuwa Mabeste hakuwa vizuri kifedha hali aliyopelekea ashindwe kuhudumia familia yake.

Ni mwaka sasa tangu kuvunjika kwa ndoa hiyo iliyodumu kwa miaka mitatu, na miaka 5 wakiwa katika mahusiano ambapo Mabeste katika mahojiano aliyofanya na B Dozen anasema kwa kipindi chote cha miaka nane aliyokuwa katika mahusiano na Lisa hajawahi kumgusa wala kumsaliti na mwanamke mwingine.

”Nadhani ishu ni pesa, inawezekana ni mwanamke mvumilivu lakini kuna wakati ulifika akachoka, akaona kwamba labda si fungu langu hapa mahali nilipo” amesema Mabeste.

Katika mahojiano hayo ametaja mambo 6 ambayo yalimuumiza sana mara baada ya kuachana na mke wake Lisa.

  1.  Mabeste anasema Lisa aliamua kumuacha na kuanza maisha mapya na rafiki yake wa karibu sana ambaye wamewahi kula mwaka mpya kwao na kutambulishwa kwa wazazi wa huyo rafiki yake, Mabeste anasema bora Lisa angeamua kwenda mbali kwa mwanaume ambaye yeye hamjui ila si kumzunguka na rafiki yake.
  2. “katika kuniacha kwake anangángánia watoto, kwahiyo naumia tena nabaki sina furaha nyingine watoto anawachukua” anasema Mabeste
  3. Ameniacha nikiwa sipo vizuri kifedha
  4. Ameenda kuishi na rafiki yangu yani anawachukua watoto anaenda kuishi nao kwa rafiki yangu.
  5. Ananiharibia mfumo wangu wa kazi sababu siwezi kufanya kazi tena na huyo rafikki yangu aliyeamaua kuishi nae kwahiyo ile nafasi aliyokuwa anafanya jamaa inabidi nitafute mtu mwingine wa kufanya nae kazi.
  6. kitu kingine kinachoniumiza ni kwamba bado haruhusu uhuru wa mimi kuwa na watoto, hataki niende kuwaangalia watoto, nikimtumia ujumbe hajibu.

Mabeste anasema jambo hili limemtesa sana hadi kufikia kipindi alitamani kufa lakini alijipa moyo kuna maisha baada ya haya.

Aidha katika kukabiliana na hayo yote Mabeste anasema alimtanguliza Mungu mbele akiamini hayo anayoyapitia ni sehemu ya maisha yake, hivyo alitumia muda mwingi kusoma neno la Mungu kama faraja kwake.

Lakini pia Mabeste anasema aliamua kukaa kimya na kuwa mtu wa kujifungia ndani kulimsaidia sana hadi sasa amesimama na nguvu zote na kurudia kazi yake ya muziki na kuzitafuta pesa kwa hasira.

 

Video: Vyombo, nguo, magodoro vyasombwa, wananchi walia umaskini
Malawi: wanafunzi watetewa na Mahakama kusokota ''dread'' shuleni

Comments

comments