Michuano ya kombe la Calabao iliendelea usiku wa kuamkia leo kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja tofauti huku vigogo wa ligi ya Uingereza wakizidi kusonga mbele kwa kushinda michezo yao.

Manchester United wakicheza katika uwanja wa Old Trafford walikuwa wakicheza dhidi ya klabu ya Burton Albion walishinda mabao 4-1, mabao ya Man Utd yakifungwa na Anthony Matrial, Jese Lingard na Marcus Rashford aliyefunga mabao mawili wakati bao la Burton likifungwa na Lloyd Dyer .

Katika uwanja wa Stamford Bridge, Chelsea walipata ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya klabu ya Nottingham Forest mabao ya Chelsea yakifungwa na Charly Musonda, Kenedy na Michy Batshuayi aliyepiga hat-trick wakati bao la Nottingham likifungwa na Teyandi Darikwa.

Manchester City waliipiga West Bromich Albion bao 2 kwa 1 huku mabao yote ya City yakifungwa na Leroy Sane na lile la Albion likifungwa na Claudio Yacob.

Chelsea ilishinda mabao 5-1 dhidi ya Nottingham Forest

Arsenal waliwapiga Doncaster Rovers bao 1 lililofungwa na Theo Walcott huku Everton wakiichapa Sunderland mabao 3 kwa 0 kupitia Calvert Lewin(2) na Bayr Oumar.

Everton ilishinda 3-0 dhidi ya Sunderland

Marcus Rashford alifunga mabao2 ktika ushindi wa 4-1 dhidi ya Burton Albion

Lema kupandishwa kizimbani oktoba 24
Video: Msigwa aelezea magumu aliyopitia Tundu Lissu, Haponi mtu