Wiki ya tafiti ya chuo kikuu cha Dar es salaam imeanza kwa ngazi ya ndani na shule kuu ya chuo hicho, kwa kuonesha kwa wadau wa tafiti, wanafunzi na wananchi kwa ujumla tafiti ambazo zimefanywa na wanataaluma wa chuo hicho ambazo zimejikita katika suala zima la maendeleo endelevu na jumuishi kama kauli mbiu ya wiki hiyo ya tano ya tafiti inavyosema.

Akiongea na waandishi wa habari naibu makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam, Tafiti na Maarifa, Profesa Cathbert Kimambo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza katika maonesho hayo ili kujifunza na kuongeza maarifa katika masula ya jamii kwa maendeleo endelevu.

Nayo taasisi ya kuthamini rasilimali ya chuo kikuu cha Dar es salaam (IRA), kupitia kwa kaimu mkurugenzi wake Dkt. Joel Norbet, amesema kuwa tafiti zinazofanywa na taasisi hiyo zinasaidia sana kuleta maendeleo katika jamii, na kuwataka wanafunzi kutoka shule na vyuo mbalimbali kuhuduria maonesho hayo.

Aidha baada ya maonesho hayo ya ngazi ya ndaki na shule kuu za chuo kikuu cha Dar es salaam kukamilika, maonesho yatakayo fuata ni yale ya ngazi ya chuo kikuu hicho kwa ujumla ambayo yanatarajia kufanyika kauanzia tarehe 6 hadi 8 mwezi ujao katika kampasi ya Mlimani.

Msimamo wa Lema, ''Sitanyamaza hata kama adhabu itakuwa mauti’’
Je unatafuta ajira?, Hizi hapa nafasi 10 za ajira kwa ajili yako

Comments

comments