Umoja wa Mataifa UN, hii leo (Oktoba 19, 2022), umetahadharisha juu ya hali ya vita katika jimbo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray kuwa inazidi kuwa mbaya na idadi ya raia wanaouwawa inaongezeka, wakati jeshi likitangaza kunyakua miji mitatu.

Serikali ya Ethiopia, ilitoa taarifa jana (Oktoba 18, 2022), ikisema jeshi lake la ulinzi limechukua udhibiti wa miji ya Shire,Alamata na Korem bila ya makabiliano katika maeneo hayo.

Hata hivyo, Jumuiya ya kimataifa imekuwa ikitoa wito wa kusitishwa katika jimbo hilo la Tigray tangu juhudi za Umoja wa Afrika za kuzileta pamoja pande zonazohasimiana kwenye meza ya mazungumzo, mwanzoni mwa mwezi huu.

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, kupitia msemaji wake Ravina Shamdasani inasema hali ni mbaya na raia wanaendelea kuuwawa.

Amesema, “Kinachotokea hivi sasa katika jimbo hilo la Tigray ni mapigano mapya katika mgogoro wa vita vya miaka miwili inavyoendeshwa na vikosi vya serikali ya Ethiopia na washirika wao dhidi ya wapiganaji wa chama cha ukombozi wa watu wa Tigray TPLF.

Mapigano mapya, kati ya vikosi vya serikali na TPLF yalianza tangu mwishoni mwa Agosti 2022, wakati pande zote mbili kila mmoja akimtupia mwenzake lawama ya kuwa chanzo cha kuvunja makubaliano ya miezi mitano ya kusitisha vita.

Marekani na Korea 'zaonesha misuli' mazoezi ya Kijeshi
Majaliwa awataka watumishi kutimiza matarajio ya Rais Samia