Imekuwa ni nadra sana kwa marais wa zamani nchini Marekani kutoa maoni yao kuhusu hali ya kisiasa chini humo kwa kuwakosoa marais wanaokuwa madarakani lakini katika utawala wa Donald Trump hali imekuwa tofauti.

Marais wawili wa zamani wa Marekani Barack na George W. Bush wameonyesha wasiwasi wao kuhusu hali ya kisiasa nchini humo bila kumtaja rais Donald Trump kwa jina.

Akizungumza wakati anamfanyia kampeni mgombea wa chama cha Democrat anayewania wadhfa wa gavana wa jimbo la New Jersey Barrack Obama aliwataka wapiga kura kukataa kile alichokitaja kuwa siasa za kuwagawanya watu.

Obama alitoa matamshi hayo saa chache baada ya George W. Bush naye kukosoa unyanyasaji na chuki katika maisha ya kawaida ya raia Marekani.

 

”Siasa tunazoziona sasa tulidhani zimepitwa na wakati, hiyo ni kurudi miaka 50 nyuma. Hii ni karne ya 21 sio 19 jamani!,” alisema Obama.

Hata hivyo rais Donald Trump ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa George Bush bado hajatoa tamko lolote.

Dar, Geita, Kagera zang'ara matokeo darasa la saba
Afisa wa tume ya uchaguzi Kenya IEBC ajiengua