Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeweka vikwazo dhidi ya Salah Gosh, mkuu wa idara ya ujasusi wakati wa utawala wa Omar al-Bashir kwa kwa kuhusika katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Sudani.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo Jumatano, Agosti 14. Salah Gosh alikuwa mkuu wa NISS, idara ya ujasusi ya Sudani katika utawala wa Omar al-Bashir.

Aidha, alijiuzulu Aprili mwaka jana, siku chache baada ya Omar al-Bashir kuondolewa madarakani na anatuhumiwa na mashirika ya haki za binadamu kuhusika na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, hasa mauaji ya wapinzani na wakosoaji wa Omar al-Bashir.

Salah Gosh, mkewe na binti yake sasa wamepigwa marufuku kuingia Marekani. vikwazo vilivyothibitishwa na duru za kuaminika kutokana na kuhusika kwake katika kesi za mateso, wizara ya mambo ya Nje ya Marekani imeeleza katika taarifa yake.

Gosh ambaye pia anatuhumiwa na shirika la kimataifa la Haki za binadamu la Human Right Watch kwa kuangamiza jamii katika eneo la Darfur, kipindi ambacho alikuwa mkuu wa NISS tangu mwaka 1999 hadi mwaka 2009, nafasi ambayo alishikilia tena mnamo mwaka 2018.

Hata hivyo, baada ya kujiuzulu kwake mnamo mwezi Aprili mwaka huu, Amnesty International ilitaka mamlaka ya mpito kuchunguza kuhusika kwake katika vifo vya waandamanaji kadhaa.

Majaliwa afichua siri kubwa kuhusu Tanzania na Afrika Kusini
Polisi wazuia mkutano wa Zitto Kabwe jijini Dar