Jeshi la Polisi nchini kupitia Kamisheni ya Polisi Jamii, limesema linaandaa mkakati na kisha kuja na mbinu ya kuzuia matukio ya uhalifu, hususani ya mauaji pamoja na ukatili.

Kamishna wa Polisi Jamii Nchini,. Faustine Shilogile ameyasema hayo wakati akizungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali mkoani Arusha hii leo Februari 16, 2023 na kusema kwasasa watahakikisha wanazuia matukio ya uhalifu kwa kuwatumia Wakaguzi wa Polisi wa Kata zote nchini.

Amesema, hivi karibuni kumeibuka matukio ya mauaji na ya ukatili wa kijinsia ambapo amesema sababu zikiwa ni pamoja na imani za kishirikina, migogoro ya ardhi na wivu wa kimapenzi, hivyo wakaguzi hao kupitia mafunzo waliyopewa wataenda kubaini viashiria vya uhalifu, kushauri na kutoa taarifa ili hatua zichukuliwe kabla ya uhalifu kutokea.

Aidha, amewataka Askari wote Nchini kwenda kushirikiana na Viongozi wa Serikali, wazee wa Mila
pamoja na viongozi wa dini, ili wote kwa pamoja wakemee vitendo hivyo pamoja na kutoa elimu kwa
wananchi ili kukomesha matukio hayo.

TASAF Malinyi yatoa zaidi ya Mil. 80 kwa kaya masikini
Mkutano AU: Rais Samia awasili nchini Ethiopia