Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema hawezi kujiuzulu nafasi yake ya Uenyekiti kwa shinikizo kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM).

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kama wanachama wa Chadema wakitaka ajiuzulu atafanya hivyo lakini sio CCM.

Amesema kazi ya Uenyekiti ni ngumu na niyakitume, hivyo ameamua kuwatumikia wana Chadema kwa nguvu zote ili waweze kufikia adhma yao.

“Siwezi kujiuzulu kwa shinikizo la CCM kwasababu najua hakuna mwana CCM anayependa Chadema iwe imara, wanapenda iporomoke, lakini kama Chadema wakitaka nijiuzulu nitafanya hivyo,”amesema Mbowe

Aidha, katika hatua nyingine, Mbowe amevituhumu vyama vingine vya upinzani kwa kushirikiana na Chama tawala (CCM) kuihujumu Chadema.

Hata hivyo, kufuatia tuhuma hizo, ametangaza kujitoa kwa Chama hicho kugombea chaguzi mbalimbali za marudio kwa madai kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi haiwatendei haki.


Video: Mgomo wa Madereva Uber wafichua yauvunguni, “Ukiwa na mgogoro na Uber suluhisho Uholanzi”

Hii ndiyo sababu Prince William kufanya mazungumzo na Rais Magufuli
Blogu yamtia mbaroni Shafii Dauda na wengine 7