Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la House on the Rock Abuja, Uche Aigbe, ameomba radhi kwa waumini wake na Dunia kwa ujumla kwa kuhubiri madhabahuni huku akiwa amebeba silaha aina ya AK-47 na kuzusha hisia tofauti.

Aigbe ameonesha kujutia kitendo hicho kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa kanisa hilo akisema alisikitishwa na nafsi yake kwa kutofikiria matokeo ya kubeba Silaha, akilenga kufafanua kifungu cha Biblia kabla ya kufanya uamuzi.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la House on the Rock Abuja.

Mchungaji huyo, aliripotiwa jinsi alivyosababisha taharuki baada ya kuonekana akiwa na Silaha hiyo madhabahuni akifafanua jambo la Kibiblia kwa minajili ya kuleta uelewa na kuhimiza waumini wake juu ya kuilinda amani.

Kipande hicho cha Video kilizua hisia tofauti kutoka kwa Wanigeria na maeneo mengine Duniani, huku baadhi ya watu wakitaka akamatwe na vyombo vya usalama na Askari aliyempatia silaha hiyo awajibishwe kwa nidhamu za kijeshi.

Mangungu: Waandishi wa Habari mnachochea
Simba SC yasisitiza ajira ya Robertinho