Taarifa tofauti tofauti kuhusu kifo cha rapa Takeoff wa kundi la Migos, zinaendelea kutoka ambapo sasa inaelezwa kuwa nyota huyo katika eneo la tukio alikuwa na rafiki zake pamoja na mwanamuziki mwenzake Quavo, ambaye licha ya mwenzie kupigwa risasi na kufariki dunia lakini yeye alibahatika kutoka salama katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa ripoti za Marekani,inaelezwa kuwa rafiki wa Takeoff, Quavo aliungana na marafiki zake wachache upande wa Kaskazini mwa Houston katika Wadi ya Tano, na saa chache baadaye, wawili hao na marafiki zao walielekea mjini Houston Kusini, kulikokuwa na mkusanyiko wa faragha kusherehekea siku ya kuzaliwa. ya Jas Prince, ambaye ni mmoja wa rafiki zao.

Hata hivyo, baada ya kutoka kwenye sherehe, indaiwa ulizuka ugomvi ambao ulisababisha milio ya risasi kurindima, na katika heka heka za ugomvi huo ndipo zilifyatuliwa risasi zilizompata rapa Takeoff na kusababisha umauti wake.

Mazingira ya kifo cha rapa huyo hayajaeleweka, lakini watu kadhaa wanadai kuwa kulitokea ugomvi walipokuwa wakicheza mchezo wa kete na akapigwa risasi kichwani au karibu na kichwa chake.

Kwa mujibu wa ripoti ya TMZ inadaiwa rapa huyo alifariki akiwa kwenye eneo latukio.

Takeoff ambaye jina lake halisi ni Kirshnik Khari Ball alizaliwa Juni 18, 1994, na anajulikana zaidi kama mwanahiphop wa kundi la Migos pamoja na mjomba wake Quavo na binamu yake Offset.

Katika hatua nyingine maafisa wa polisi huko Houston, wametoa wito kwa wananchi kuisaidia polisi kwa namna yeyote ilikuhakikisha muhusika wa mauaji hayo anatiwaa nguvuni ili kujibu mashtaka yanayomkabili.

Kifo cha mtoto 'swiming pool': Polisi yawashikilia wafanyakazi wa Davido
Wanajeshi wa Kenya 'wajipanga' kuwakabili M23