Uzinduzi wa wimbo wa Harmonize ‘Uno’ uliofanyika usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam ulikuwa wa kipekee ukisindikizwa na ‘mastaa mbalimbali’ wa Bongo Fleva na waigizaji, na mmojawapo alikuwa Menina ambaye aliweka alama ya aina yake jukwaani.

Mrembo huyo ambaye wiki kadhaa zilizopita alizua mijadala mingi na hata kufika mbele ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kujieleza kufuatia video zake za faragha kuvuja, alionekana akiwa mwenye furaha wakati wote kwenye meza aliyosimama na warembo kadhaa akinywa ‘vimiminika’ huku akivutwa na hisia za muziki mzuri kutoka kwa Harmonize.

Hata hivyo, jicho la mwanafamilia huyo wa zamani wa WCB liliuona mzuka wa mrembo huyo na kumtaka afike jukwaani awape ladha kidogo mashabiki waliofika kushuhudia uzinduzi wa ‘Uno’. Msanii huyo alifunguka na kuitendea haki ‘Uno’ kwa sekunde kadhaa akiongozwa na Harmonize jukwaani hapo, alizungusha alichojaliwa kuwa nacho, hali iliyozua shangwe kubwa.

Hii inaonesha kuwa msanii huyo ambaye awali aliripotiwa kuwa katika wakati mgumu kisaikolojia amepata tiba mahsusi na ameamua yaliyopita si ndwele anaendelea na maisha katika mlengo chanya.

Baadhi ya wasanii waliopanda kwenye jukwaa kumuunga Mkono  Harmonize ni pamoja na Q Chillah, Marioo, Linah na wengine.

sekta ya maendeleo ya jamii kusimamia mfuko wa bima ya afya
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 25, 2019