Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi kwa mara ya kwanza amemfunga mlinda mlango wa Juventus na timu ya Taifa ya Italia Gianluigi Buffon katika mchezo wa ligi ya mabigwa ambapo Barcelona iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Juventus.

Messi alianza kuzifumania nyavu dakika ya 45 kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika. Ivan Rakitic alifunga bao lingine la Barcelona dakika ya 56 kabla ya Messi kumfunga tena Buffon  bao lake la pili dakika ya 69 ikiwa ni mara ya kwanza kwa Messi kumfunga kipa huyo tangu wakutane katika michezo mitatu iliyopita.

Mabao mawili ya Lioneil Messi yanamfanya kufikisha idadi ya mabao 59 katika hatua ya makundi ya michuano ya Champions League na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi katika hatua ya makundi.

Messi ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Barcelona mpaka sasa amefunga mabao nane katika michezo sita aliyokwisha cheza kwenye michuano yote msimu huu.

Messi hakuwahi kumfunga Buffon katika michezo mitatu waliokutana

Juventus waliitoa Barcelona katika robo fainali ya michuano ya klabu bingwa msimu uliopita kabla yakutinga fainali ambapo walifungwa na Real Madrid.

 

 

 

 

 

Video: Zitto, Kubenea kitanzini, Jinsi Meja Jenerali alivyopigwa risasi akitoka benki
Rufaa ya Sadio Mane yagonga ukuta