Mamilioni ya wasafiri nchini Ujerumani, hii leo Jumatatu Machi 27, 2023 wamelazimika kutafuta njia mbadala ya usafiri baada ya kushuhudiwa kwa mgomo katika sekta ya uchukuzi.
Viwanja vya ndege, vituo vya mabasi, treni na njia za majini kote nchini humo vilikuwa vitupu kufuatia mgomo huo unaotajwa kuwa mkubwa zaidi tangu miaka ya 1990.
Katika mgomo huo utakaodumu kwa saa 24 kuanzia leo wafanyakazi milioni 2.5 wa Shirikisho na Manispaa, Chama cha Wafanyakazi Verdi na Chama cha Wafanyakazi wa UMM DBB wanadai nyongeza ya mshahara ya asilimia 10.5.
Treni za masafa marefu, zimeahirisha safari zake,hatua iliosababisha usumbufu kwa mamilioni ya watumiaji wa huduma hiyo muhimu,hasa katika majimbo kadhaa makubwa.
msururu wa magari ya madogo, yakitumika kama mbadala wa usafiri umeshuhudiwa wenye matokeo ya uchelewaji barabarani kama matokeo ya mgomo wa siku ya Jumatatu.
Wawakilishi wa Verdi na DBB wanatarajiwa kukutana tena na maafisa wa serikali leo Jumatatu kwa duru ya tatu ya mazungumzo.