Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amewasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2022 hadi 2023 kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira hii leo Machi 27, 2023 Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Jackson Kiswaga kwa niaba ya Kamati amekiri kupokea taarifa hiyo.

Aidha, Kiswaga amefafanua mambo mbalimbali juu ya hatua zinazofuata kwenye kikao cha Kamati hiyo kilichoketi hii leo Jijini Dodoma ili kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2022 hadi 2023.

Waziri Mkuu: Maafisa Habari ongezeni ubunifu
Mgomo usafiri wa Umma waisimamisha Ujerumani