Aliyekua kiungo na nahodha wa kikosi cha Arsenal, Mikel Arteta anatarajiwa kutangazwa kuwa meneja msaidizi wa kikosi cha Man City wakati wowote juma hili.

Kiungo huyo kutoka nchini Hispania amefikia hatua nzuri za mazungumzo na uongozi wa klabu ya Man City, baada ya kupendekezwa na meneja mkuu Pep Guardiola aliyetokea kwa mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich.

Arteta, amejitumbukiza katika ukufunzi wa soka baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Arsenal mwishoni mwa msimu uliopita na inaaminika ameachana na masuala ya kucheza soka (Amestaafu).

Hata hivyo Arteta mwenye umri wa miaka 34, alitarajiwa huenda angekua kocha wa timu ya vijana ya Arsenal, lakini taarifa za kuwa mbioni kufanya kazi na Guardiola zinahitimisha mpango huo.

Louis van Gaal Afikiriwa AC Milan
Antonio Conte Ajipanga Kuwahamisha Candreva, Bonucci