Drama iliyopikwa kutoka kwenye uhusiano wa kimapenzi uliokuwa na ‘mbwembwe’ za kila aina kati ya Shilole na Nuh Mziwanda inaendelea kupewa nafasi kutokana na utata wa ushindani unaoibuka.

Mrembo anayefanana na Shilole aliyetumika kwenye video ya wimbo mpya wa Nuh Mziwanda aliomshirikisha Ali Kiba ‘Jike Shupa’, amejitokeza na kumvimbia Shilole kuwa anamfunika kwa uzuri na urembo.

Mrembo huyo anayeitwa Zuwena ameiambia Clouds TV kuwa yeye ni mzuri kuliko Shilole licha ya kufananishwa naye.

“Kwakweli mimi namuona wa kawaida tu. Akumbuke na mimi mzuri kuliko yeye,” Zuwena alivimba.

Shilole aliwahi kudai kuwa yeye ndiye mwimbaji wa kike mzuri zaidi ya wote.

Nuh Mziwanda na Shilole kabla ya kuachana

Nuh Mziwanda na Shilole kabla ya kuachana

Katika video ya Jike Shupa, Nuh amejaribu kuonesha jinsi ambavyo maisha yake na Shilole yalivyokuwa yamejaa unyanyasaji wa ‘kijinsia’ dhidi yake.

Simba Yaendelea Kuifumua Mtibwa Sugar
Video: Ilala imekuja na hii ripoti ya matukio ya kikatili kwa watoto ndani ya miaka mitatu