Rais wa Malawi, Dkt. Lazarus Chakwera amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Wananchi wa Tanzania kwa msaada uliowasilishwa kwa niaba yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax kutokana maafa yaliyoikumba nchi hiyo ya kimbunga Freddy.
Rais Chakwera ametoa shukrani hizo hii leo Machi 20, 2022 na kueleza furaha yake kwamba msaada huo umewafikia kwa haraka na kwa wakati huku akisema hiyo ishara ya undugu na mshikamano uliopo kati ya Tanzania na Malawi.
Amesema, ” kama mtakumbuka kwamba hii si mara ya kwanza kwa Tanzania kuisiadia Malawi kwani iliwahi kufanya hivyo mwaka 2015, mwaka 2019 na mwaka huu 2023 kutokana na maafa yaliyotukumba.
Msaada wa kibinadamu uliotolewa ni pamoja na fedha taslim na vifaa mbalimbali wenye ya thamani ya Dola za Marekani Milioni Moja, chakula, vifaa vya kuokolea, vifaa vya kujihifadhi, Helikopta 2 za kijeshi zitakazotumika kupeleka misaada katika uokoaji pamoja na wanajeshi 100 watakaoshiriki kusambaza msaada huo, Mahema 50, Blanketi 6,000, Tani 1,000 za unga wa mahindi na fedha taslim kiasi cha Dola za Marekani 300,000.