Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) limetangaza majina sita ya waamuzi  watakaochezesha mtanange wa watani wa jadi kati ya Simba SC dhidi ya Young Africans utakaopigwa Jumamosi (Mei 08) Uwanja wa Benjamini Mkapa, jijini Dar es salaam.

Simba SC inyoongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara itakuwa mwenyeji wa mchezo huo,ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini nap engine Afrika mashariki na kati.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na TFF kwenda kwa vyombo vya habari  iliwataja waamuzi hao kuwa ni Emmanuel Mwandembwa (wa kati), Frank Komba (Msaidizi 1), Hamdani Saidi( Msaidizi 2), na Ramadhani Kayoko( Akiba).

Waamuzi hao watahakikisha sheria 17 za mchezo wa soka zinafuatwa kikamilifu kwenye mpambano huo ambao umepangwa kuanza mishale ya saa kumi na moja jioni.

Simba SC inaongoza msimamowa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 61, ikifuatiwa na Young Africans yenye alama 57 huku Azam FC wakishika nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 54.

Coastal Union: Mgunda hajafukuzwa
Bill Gates na mkewe waachana rasmi