Ndoa ya Tajiri wa Dunia Bill Gates na Belinda iliyodumu kwa miaka 27 na kupata Watoto watatu imetangazwa kufika mwisho na sasa kila mmoja anaanza maisha mapya baada ya kuachana.

Taarifa iliyotolewa leo na mke wa Gates imesema wawili hao wamefikia maamuzi ya kuvunja ndoa hiyo lakini wataendelea kushirikiana kwenye kazi zinazohusu foundation yao ambayo imekua ikitoa misaada kwa Nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania.

Ndani ya miaka mitatu hii inakua ndoa ya Tajiri mwingine wa dunia kuvunjika ambapo talaka ya Tajiri Jeff Bezos ilitangazwa April 2019 wakiwa wamedumu kwa miaka 25 kwenye ndoa na kupata Watoto wanne.

Mwandembwa kupuliza filimbi Mei 08
Jafo aagiza kukamatwa Mkurugenzi aliyetelekeza makontena