Mwimbaji mkongwe ambaye alikuwa kiongozi wa kundi kongwe la Rock la Motorhead, Lemmy Kilmister amefariki jana, Desemba 28 majira ya saa kumi jioni akiwa na umri wa miaka 70.

Ripoti zinaeleza kuwa  saratani ndio chanzo kikuu cha kifo chake na kwamba alizidiwa siku mbili zilizopita na kukimbizwa hospitalini alipolazwa hadi umauti ulipomfika.

Mwimbaji huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa muda mrefu na uvutaji wa sigara ndio unaodaiwa kuwa chanzo cha ugonjwa huo. Amekuwa akivuta sigara kwa takribani miaka 57 ya uhai wake.

Alizaliwa Staffordshire nchini Uingereza mwaka 1945. Alitumia muda mwingi wa maisha yake kujihusisha na muziki wa bendi uliompa umaarufu mkubwa. Mwaka 1975 alianzisha kundi la Motorhead nchini Uingereza.

Arsenal Imeanza Msako Wa usajili Wa Januari 2016
Hanspope Wa Simba Azushiwa Jambo Zito