Mshindi wa Tuzo za Muziki za Kilimanjaro, Barakah Da Prince  ameweka wazi nia yake ya kumpa ajira ya ualimu mtu atayekuwa na vigezo vya kumnoa kuzungumza kiingereza ili aende sawa na vyombo vya habari vya kimataifa bila mkalimani.

Akifunguka leo kupitia E-FM, Mwimbaji huyo wa ‘Nivumilie’ amesema kuwa alipata changamoto ya lugha alipofanya mahojiano yake ya kwanza makubwa na kituo cha MTV kuhusu wimbo wake mpya wa ‘Nisamehe’, hali iliyopelekea kutumia Kiswahili akiwa na mtafsiri wake pembeni.

“Niliulizwa kwenye interview ya MTV kama naweza kuongea Kiingereza, nilichowajibu naweza ila sio Kiingereza kilichonyooka ndio maana nikatumia Kiswahili. Nafurahi kwa kuwa walivutiwa na Kiswahili,” alisema Barakah Da Prince.

Aliongeza kuwa ingawa mpenzi wake Naj ni mkali wa ‘yai’, ameshindwa kumfundisha kutokana na kuwa na masihala mengi pindi somo hilo linapoanza hali iliyomlazimu kumsaka mwalimu.

“Hanifundishi lugha kwa sababu tuna masihala mengi hivyo nahitaji mtu ambaye atakuwa serious,” alisema.

Tofauti na wawili hao, Diamond Platinumz ni mmoja kati ya wasanii ambao walianza kufanya muziki bila kuifahamu lugha ya Kiingereza lakini alipikwa na  aliyekuwa mpenzi wake, Wema Sepetu na kuweka bidii. Hivi sasa mkali huyo wa Ngololo anaijua lugha hiyo ya kigeni kama ‘kizaramo’ cha kwao.

Gavana BOT afichua siri ya kilio cha fedha kupotea mtaani
Bodi ya Filamu kutoa ushirikiano uanzishwaji wa Mradi wa TYEEO