Klabu ya Namungo FC imethibitisha kupokea barua kutoka Shirikisho la soka duniani FIFA, ambayo imethibitisha adhabu ya kufungiwa kwa mshambuliaji wao Shiza Ramadhan Kichuya kwa muda wa miezi sita.

FIFA walitangaza adhabu hiyo mwanzoni mwa juma hili, baada ya kutoa hukumu ya kesi iliyowasilishwa kwao na klabu Pharco ya Misri, ambayo mshambuliaji huyo aliwahi kuitumikia akitokea Simba SC.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino Namungo FC, Kidamba Namlia amesema barua iliyotumwa klabuni hapo kwa njia ya Barua Pepe (E-mail), ilikuwa ina maagizo kwao pamoja na Simba SC ambao waliokuwa waajiri wake wa zamani.

“Kuhusu masuala ya wachezaji mimi huwa ninasimamia kila kitu na nilipokea barua kwa njia ya email ambayo imetutaka tusimtumie mchezaji Kichuya, (Shiza) mpaka pale ambapo mabosi wake wa zamani watalipa faini.

“Kufungiwa kwa Kichuya kwetu ni pigo kwa kuwa Simba kwa sasa hawana hesabu naye hasa kwa kuwa walimuacha na ni mchezaji huru, sisi tayari alishaingia kwenye mfumo.

“Adhabu hiyo ikiwa haitatekelezwa na Simba basi kuna uwezekano wa mchezaji huyo kufungiwa kucheza ikiwa haitalipwa kwa wakati,” amesema.

Kichuya amekutana na adhabu hiyo kutoka FIFA kwa kufungiwa kutocheza mpaka pale Simba itakapolipa faini ya Shilingi milioni 300, baada ya kumsajili mchezaji huyo kinyume na utaratibu wa kimkataba.

Kichuya alisajiliwa na mabosi wake wa zamani Simba ambao walimuuza nchini Misri kutoka Klabu ya Pharco ambayo imedai kuwa alikatisha mkataba ndani ya timu hiyo na kuibukia Simba.

Flick: Robert Lewandowski atakua 'FIT'
UNEP yatahadharisha ongezeko la joto Duniani 

Comments

comments