Mwimbaji wa Kivuruge, Nandy amezungumzia mpango wa kufanya kazi na wasanii wa kimataifa ikiwa ni pamoja na wasanii wawili wakubwa wa Nigeria na msanii mmoja wa kike gwiji wa Marekani.

Mkali  huyo aliyechomoza kupitia shindano la ‘Tecno Own the Stage’ miaka kadhaa iliyopita amesema kuwa mpango wa kufanya kazi na Yemi Alade pamoja na Wizkid uko palepale lakini ana sababu ya kuuchelewesha.

Alisema angependa kuona anajikuza yeye kwanza bila kutegemea wasanii wengine kwenye nyimbo zake ili wanapokutana kwenye wimbo mmoja wanakuwa wasanii wakubwa waliokutana, na sio msanii mkubwa akimsaidia msanii mdogo.

“Sitapenda ifike hatua watu waseme ‘Nandy bila yule’asingefika hapa. Kwahiyo najaribu kusimama Nandy kama Nandy nione kama kwenye YouTube yangu naweza kufikisha viewers milioni 5 kama wengine na kuendelea,” Nandy aliiambia The Playlist ya Times Fm.

“Nijenge ule ukubwa ili angalau baadaye hata nikifanya kazi na Yemi, [halafu aseme] kama ‘jamani yule ni msanii mdogo wa Tanzania nimemsaidia’. Iwe kama ‘nimefanya kazi na mmoja kati ya wasanii wenye fanbase yake na tukikutanisha yeye anapata na mimi napata’,” alisema Nandy.

Akizungumzia kama kuna mpango wa kufanya kazi na Rihanna! Swali alilotupiwa na Lil Ommy kufuatia tetesi kuwa kuna ‘collabo’ nzito na msanii wa kike wa Marekani, alijibu, “Rihanna…!! [anacheka]. Rihanna bado kwakweli, lakini yupo msanii wa Marekani ambaye ndio tunakaribia, ni msanii mkubwa na gwiji wa Marekani. Ni mkubwa sana na gwiji.”

Ingawa hakumtaja jina msanii huyo wa kike wa Marekani, alisisitiza kuwa collabo na Wizkid na Yemi Alade ipo.

Mayweather kupigana Tokyo kabla ya kunyukana na Pacquiao
Serikali haina mtandao wa kutoa mikopo kwa dakika 45