Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema ndoto ya Tanzania kuuza umeme wake nje ya nchi bado ipo, ingawa ni lazima kujiridhisha kwenye mambo kadhaa kabla ya kufikia uamuzi huo.
Makamba ameyasema hayo Bungeni kwenye maonyesho ya Wiki ya Nishati na kuongeza kuwa ni kweli suala la Umeme bado halijatengemaa lakini kupitia mpango huo litatimia.
Amesema, “kwanza ni lazima umeme wetu uwe umejitosheleza kwa watu wetu wa ndani, pili Kujenga inter connector ambapo kwa sasa vitu vyote hivyo viwili bado havijakamilika.”
Kuhusu uzalishaji wa umeme nchini, Waziri Makamba amesema umeongezeka kwa asilimia 11 kwa mwaka, ambapo awali kulikua ongezeko la asilimia 5 kwa mwaka jana (2022), na kwa mara ya kwanza wanakaribia kuongeza asilimia 10.