Wakati zoezi la kupiga kura likiwa limefungwa na zoezi la kuhesabu kura linaendelea katika baadhi ya vituo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imelazimika kuahirisha uchaguzi katika baadhi ya maeneo hususan jijini Dar es Salaam kutokana na changamoto zilizopelekea wananchi wengi kushindwa kupiga kura.

Akiongea na waandishi wa habari jioni hii, Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima alisema kuwa kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika vituo vya vya Kimara Stop Over jijini Dar es Salaam, wamelazimika kuahirisha zoezi la upigaji kura katika eneo hilo hadi hapo kesho.

Wananchi katika eneo la Kimara Stop over waliojiandisha katika daftari la kupiga kura lakini walishidwa kupika kura kwa kile kilichooelezwa kuwa ni ukosefu wa vifaa vya kupigia kura pamoja na kukosa wasimamizi wa NEC wa kutosha katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa takwimu, watu takribani 12,000 hawakuweza kupiga kura katika eneo hilo la Kimara Stop Over.

Maeneo mengine ambayo yameripotiwa kuwa na changamoto za wananchi kushindwa kupiga kura ni baadhi ya vituo katika eneo la Kinondoni, Mbagala na Mburahati.

 

 

Wagombea Ubunge Waliojitangazia ushindi na Hali ya Baadhi ya Majimbo
Magufuli: Matone Ya ‘Mvua’ Yamenidondokea