Saa chache baada ya zoezi la kupiga na kuhesabu kura kukamilika katika maeneo mengi nchini, taa ya kijani kuelekea Dodoma imeanza kuonekana kwa baadhi ya wagombea ubunge ambao wamejitangaza kufuatia matokeo ya awali.

Baadhi ya wagombea wameyatumia matokeo ya awali yaliyotangazwa na kubandikwa katika vituo vya kupigia kura.

Mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ni mmoja kati ya wagombea waliojitangaza mapema jana jioni.

Hata hivyo, matokeo ya awali yameanza kuonesha ishara nzuri kwa baadhi ya wagombea ubunge wa Ukawa waliotajwa kuwa wanaongoza ni pamoja na Ester Matiku (Tarime Mjini), Ester Bulaya (Bunda Mjini), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Wilfred Lwakatare (Bukoba Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki).

Majimbo ya Ilemela na Nyamagana jijini Mwanza yanaonekana CCM inaongoza ikiwa imechukua kata nyingi zaidi. Jimbo la Musoma Mjini linaonekana kuwa na dalili zote za kuwa mikononi mwa CCM hivi sasa kwani matokeo ya awali yanaonesha kata 14 kati ya 16 zimeshikiliwa na CCM.

NEC inatarajia kutanganza matokeo rasmi leo kuanzia saa tatu asubuhi na lolote linaweza kutokea kwani hayo ni matokeo ya awali. 

Ester Matiko Atangazwa Rasmi Kuwa Mbunge Wa Tarime Mjini
NEC Yaahirisha Uchaguzi Baadhi Ya Maeneo