Elimu ya watu wazima ‘Ngumbaru’ imetajwa kuwa kiungo muhimu kwenye mipango ya maendeleo ya taifa kwa wtu wasiojua kusoma na kuandika ili kushinda vita ya harakati za kuimarisha huduma za jamii.
Hayo yamebainishwa katika ripoti ya Umoja wa mataifa kupitia lengo lake la 4 la maendeleo endelevu SDGs, inayopania kuhakikisha elimu inapatikana kwa watu wote Duniani.
Malengo hayo ya kielimu, ya kuwaelimisha watu wazima yanashabihiana na lile la 4 la malengo ya malengo endelevu ya Umoja wa mataifa, SDGs la kuhakikisha elimu inapatikana kwa wote na kuimarisha juhudi za kuwasomesha wahitaji.
Kulingana na kiashiria cha nne, cha lengo la 4 la SDGs la kuhakikisha elimu kwa wote maishani, azma ya UN ni kuiongeza idadi ya vijana na watu wazima walio na elimu ya kiufundi au taaluma ifikapo mwaka 2030.