Timu ya taifa ya vijana ya Nigeria chini ya miaka 17 (Golden Eaglets) imetwaa ubingwa wa kombe la dunia kwa vijana.

Nigeria imeibamiza timu ya taifa ya vijana ya Mali 2-0, katika mchezo wa hatua ya fainali ya michuano hiyo iliyokua ikiunguruma nchini Chile.

Mshambulia Victor Osimhen ndie aliyeanza kuipatia timu yake bao la kwanza na Funsho Ibrahim Bamgboye akaongeza bao la pili na la ushindi.

Kikosi cha cha vijana cha Nigeria kimeweza kutetea ubingwa wake baada ya kutwaa taji hilo la dunia la vijana mwaka 2013 walipoibanjua timu ya taifa ya vijana ya Meixco kwa ushindi wa mabao 3-0.

Mshambuliajia Victor Osimhen ameibuka fungungaji bora wa kihistoria kwa kuzichezea nyavu za wapinzani mara 10 kwenye michuano hiyo ya kombe la dunia kwa vijana mwaka 2015.

Fainali zijazo za kombe la dunia kwa viojana chini ya umri wa miaka 17, zimepangwa kufanyika nchini India kuanzia August 19 hadi  Septemba 10.

Mmiliki Wa Chelsea Amfungia Vioo Jose Mourinho
TP Mazembe Mabingwa Afrika 2015