Rapa wa Weusi, Nicki wa Pili amesema kuwa kundi hilo halikuwa na lengo la kuwaeleza mashabiki wake kuhusu collabo kati ya Joh Makini na mkali wa ‘Skelewu’, Davido.

Hata hivyo, Davido alikuwa mtu wa kwanza kuweka hadharani collabo hiyo kupitia akaunti yake ya Twitter, huenda baada ya kuona kazi hiyo ni moja kati ya kazi kubwa ambazo mashabiki wao inabidi wakae mkao wa kula kukipokea.

“Unajua Davido aliibreak ile news. Sisi tulitaka iwe kimya kimya, ilikuwa bado iko undercover. Lakini suddenly Davido alitweet jana na issue ikaenda viral so tukawa hakuna jinsi, lakini bado sio mbaya,” alisema Nikki wa Pili.

Alisema kuwa chanzo cha collabo hiyo ni juhudi za Joh Makini mwenyewe ambaye alikuwa akiifuatilia na kuwasiliana na Davido muda mrefu kuhusu huo mpango. Aliongeza kuwa bado mambo mengi makubwa yanakuja kutoka kwenye kundi hilo. Bila shaka ana maanisha collabo nyingi kubwa za kimataifa.

Weusi wanaendelea kuvuka mipaka na kufanya collabo na wasanii wakubwa, hivi karibuni Joh Makini alifanya collabo na rapa mkubwa wa Afrika Kusini, AKA.

Lowassa: Mungu Anipe Nini Miye…
NCCR- Mageuzi Waeleza Njama Za Kumuua James Mbatia