Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza amesema kuwa hakuna mwanajeshi wa Umoja wa Afrika (AU) atakayeingia nchini kwake kwa ajili ya oparesheni iliyotangazwa hivi karibuni na umoja huo.

Akiongea jana nchini humo na ujumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Umoja wa Mataifa, Nkurunzinza alisisitiza kuwa Umoja wa Afrika unapaswa kuiheshimu Burundi kama nchi mwanachama na inatakiwa kujadili nayo kwa suala hilo.

“Watu wa Burundi waliamua kupitia Bunge lao, AU lazima waiheshimu Burundi kama nchi mwanachama na tunapaswa kushirikishwa,” alisema Nkurunzinza.

AU ilitangaza hivi karibuni mpango wake wa kupeleka kikosi chenye nguvu cha wanajeshi 5,000 watakaosaidia katika kurejesha na kulinda amani nchini humo.

Hadi sasa watu zaidi 439 wanaripotiwa kufa kutokana na machafuko humu zaidi ya watu 220,000 wakikimbia nchi hiyo. Machafuko ya kisiasa nchini humo yanatokana na uamuzi wa rais Nkurunzinza kugombea tena urais kwa muhula wa tatu, kinyume cha katiba ya nchi hiyo.

Diamond adai mtoto wake anawazidi pesa wasanii hawa wa Bongo
'Magufuli atauwa vyama vya upinzani nchini'