Diamond amechoshwa na majungu yanayopikwa kwa mtoto wake Tiffah na baadhi ya wasanii wakubwa na sasa ameamua kuwatolea uvivu.

Akiongea na Ayo TV, Diamond amewataka wasanii hao kuachana na mtoto wake kwa kuwa mtoto huyo hawahusu na badala yake wajikite katika kutafuta fedha wapate mafanikio.

TIFFAH

Alisema wasanii hao wanaohangaika na mtoto wake, wanaweza kuwa wanazidiwa fedha na mtoto huyo.

Hivi ndivyo alivyosema:

“Watu wamekaa kwenye sanaa muda mrefu mimi nimewakuta, nawaona wameanza kuwa mastaa kabla ya mimi, hawana viwanja, hawana nyumba, hawana magari. Wangetumia muda huo kutengeneza maisha yao kuliko kukaa kumdis mtu mwingine. Halafu mimi sipendagi kusema lakini inavyofika hatua kwenye vitu kama hivi mimi naongea. Kwanza nilikuwa sijui uchungu wa mtoto sasa hivi naujua kwamba kweli mtoto anauma

“Halafu mtu anayezungumzia inawezekana mtoto akawa na pesa kuliko hata yeye, kwa sababu akaunti ya Tiffah inawezekana ikawa na hela hata kuliko huyo mtu anayemdiss huyo mtoto kama sio wangu mimi. Inawezekana akawa na hela kuliko hata wewe unayesema mtoto sio wangu au unasema mtoto mbaya. Kwa sababu mtoto alifunguliwa akaunti yake kwa mara ya kwanza ikaingia milioni 10. Ni mtoto inawezekana ni maarufu kuliko hata wewe kwa sababu nikifika Nigeria wanaanza kuuliza Tiffah hajambo? So inafikia time hata kwa mtoto unataka kiki?”

Membe aunga jambo 'kilio' cha Lowassa
Nkurunzinza 'awatupa' nje ya Burundi wanajeshi wa Umoja wa Afrika