Mshambuliaji wa Simba raia wa Uganda, Emmanuel Okwi, ameshangazwa na uongozi wa timu yake kwa kushindwa kusajili mchezaji yeyote mpya mpaka sasa.

Okwi amesema siku za usajili zimebaki nne kabla dirisha dogo la usajili kufungwa na anashangazwa kuona mambo yapo kimya.

“Nimepata hofu baada ya kuona siku zinakwenda halafu hakuna usajili wowote ambao tumeufanya wakati wapinzani wetu kwenye mbio za ubingwa Yanga na Azam FC wamesha sajili wachezaji watatu Hadi wawili,” alisema Okwi.

Mshambuliaji huyo amesema kama wanashindwa kusajili anahofia mambo kuzidi kuwawia magumu na hata kushindwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu kwani ushindani umekuwa mkubwa tofauti na matarajio yao wakati wanaanza msimu.

Awali kulikua na tetesi kuwa klabu hiyo itamsajili beki na nahodha wa Lipuli FC Asante Kwasi lakini inaonekana tofauti kwani Hadi sasa mambo yapo kimya .

Simba imepanga kuongeza wachezaji wanne kwenye dirsha dogo wachezaji hao ni kipa mmoja beki wa Kati mmoja na brki wa pembeni mmoja na mshambuliaji mmoja.

 

West Ham Utd wamshtua Antonio Conte
Europa League: Arsenal wapangiwa Ostersunds