Kocha Mkuu wa Simba SC Franco Pablo Martin amesema tayari amewakabidhi ripoti viongozi wa klabu hiyo na anahitaji wachezaji watano ambao watasaidia timu hiyo kufiki malengo yao waliyojiwekea msimu huu 2021/22.

Kocha Pablo amesema katika ripoti yake ameshaikabidhi kwa viongozi, amependekeza usajili wa beki na viongo ambao wataongeza uhai kwenye kikosi chake, ambacho kinakabiliwa na mtihani wa kutetea taji la Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Nafasi za awali ni beki na viungo ambao watakuja kuleta ushindani mkubwa kwa wachezaji waliopo na kusaidia timu kufikia malengo yetu,” amesema kocha Pablo.

Simba SC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa alama tano nyuma ya Young Africans inayoongoza msimamo huo na alama zake 29, baada ya kushuka dimbani mara 11 huku Wekundu wa Msimbazi hao wakiwa mchezo mmoja nyuma.

Kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba SC ipo Kundi D pamoja na Asec Mimosas ya Ivory Coast, RS Berkane (Morocco) na USGN ya Niger.

Mkwasa arudi Ruvu Shooting
Kampuni ya ‘Apple’ yavunja rekodi