meneja wa klabu bingwa nchini  Ujerumani, FC Bayern Munich, Pep Guardiola amesema kuwa ataamua mustakabali wa maisha yake ndani ya klabu yake ndani ya msimu ujao.

Kocha huyo ambaye kwa sasa ndiye bidhaa adimu katika soka la Ulaya kwa upande wa makocha,amesema kuwa bado hajafikiria ni nini kitafuata baina yake na klbau hiyo ambayo amejiunga nayo katika misimu minne iliyopita.

Amesema kuwa anaamini maamuzi atakayochukua juu ya hatma yake katika klabui hiyo yatamfurahisha kila mmoja huku akisisitiza kuwa hatafurahishwa kama kuna upande utahuzunika kwa mamamuzi hayo.

Taarifa za ‘chini ya kapeti’ zinasema kuwa huenda kocha huyo akaamua kutoongeza mkataba wa kuendelea kuifunza timu hiyo ambayo imekuwa bingwa katika kipindi chote ambacho amekuwa nayo nchini Ujerumani.

Aidha taarifa zinasema kuwa huenda kocha huyo wa kukumbukwa katika klabu ya Fc Barcelona akajiunga na moja wapo ya timu kubwa za Uingereza huku timu toka jiji la Manchester zikipewa nafasi kubwa ya kumsaini.

Taarifa nyingine zinadai kuwa Klabu hiyo imeanza mazungumzo ya chini chini na aliyekuwa kocha wa Madrid,Carlos Ancelotti kwa ajili ya kwenda kuinoa timu hiyo endapo Pep atatangaza kuhama katika timu hiyo.

Mfahamu Mkali Wa Mabao Ligi Ya England, Jamie Vardy
Mourinho Kuendelea Na Maisha Yake Jijini London