Kikosi cha Simba SC kimewasili salama mjini Casablanca nchini Morocco tayari kwa mchezo wa mwisho wa Kundi C, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Raja Casablanca.

Simba SC yenye alama 09 itacheza mchezo huo huku ikiwa tayari imeshapata tiketi ya kucheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, sambamba na wenyeji wao Raja Casablanca wanaoongoza msimamo wa Kundi C kwa kufikisha alama 13, baada ya kucheza michezo mitano.

Vyanzo vya habari vya Simba SC vimethibitisha kuwasili salama wa kikosi cha klabu hiyo, ambacho kililazimika kusitisha safari kwa muda baada ya Ndege wa shirika la Ndege la Qatar kupata hitalafu katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro ‘KIA’ juzi Jumanne (Machi 28).

Hata hivyo katika msafara uliowasili mjini Casablanca wachezaji waliokuwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania ‘TAIFA STARS’ nao wameonekana wakiwa sambamba na wale waliotangulia kuondoka nchini.

Ushindi ni kama kunywa maji Meridianbet kasino ya mtandaoni
Nagelsmann aziingiza vitani Chelsea, Tottenham