Vikosi vya Usalama nchini Kenya viko katika hali ya ulinzi mkali na tahadhari baada ya kupokea taarifa za ujasusi kwamba wanamgambo wamekuwa wakipanga mashambulizi ya kigaidi wakati au baada ya sikukuu ya Pasaka.

Hayo yamethibitishwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kenya, George Kinoti ambapo ameeleza kuwa wamepokea taarifa za ujasusi zikieleza kuwa wanamgambo tisa wanapanga mashambulizi, hivyo tayari vikosi vya usalama vimejiimarisha na kuhakikisha kunakuwa na tahadhari ya juu kudhibiti mashambulizi yasitokee.

Jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi wote kuwa waangalifu kwa hali ya juu kabla ya sikukuu ya Pasaka na kuripoti shughuli zote watakazozitiliwa shaka.

Serikali yazidi kuwabana wakwepa kodi
Mourinho Awachana Washambuliaji Man Utd