Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam limesema kuwa limejipanga ipasavyo kuhakikisha mchezo wa Yanga dhidi ya Mo Bejaia leo (13/08/2016) wenye mvuto mkubwa wa mashabiki wa Tanzania, Afrika mashariki na Afrika nzima unachezwa katika hali ya usalama na amani.

Akizungumza hayo mbele ya waandishi wa habari, Naibu Kamishna wa polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, DCP Hezron S. Gyimbi amewataka wananchi kutokuwa na shaka yoyote ya kiusalama na pia kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kwa jambo lolote wataloliona kuwa linaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani kwa kipindi chote watakapokuwa nje au ndani ya uwanja.

DCP Hezroni amesema kutakuwa na CCTV Camera ili kuhakikisha sehemu zote, mageti ya kuingilia na kutokea yanaonekana na kuweka kumbukumbu za matukio yote.

Aidha jeshi hilo limewataka wananchi kuwa watulivu katika kushangilia mechi hiyo na kuepuka kufanya mambo haya:

  • Kuingia na chupa za kimiminika cha aina yoyote
  • Kuingia na silaha ya aaina yoyote
  • Kupaki magari ndani ya uwanja
  • Kukaa sehsmu ambazo tiketi zao haziwaruhusu.

Maalim Seif amtembelea Ndugai nyumbani kwake
Video: Rais Magufuli atangaza kuchambua 'nukta kwa nukta', Aitaja UVCCM