Baadhi ya Maafisa wa Polisi wanashukiwa kuwalinda wahalifu na hivyo kuchangia kuzuka upya kwa magenge ya kiuhalifu jijini Nakuru nchini Kenya.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Kaunti ya Nakuru, Loyford Kibaara amesema uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya maafisa wa Polisi katika maeneo ya Rhonda na Kaptembwa wanashirikiana na magenge ya wahalifu.

Eneo la Kivumbini Estate – Nakuru nchini Kenya.

Amesema, hali hiyo imekuwa ikitatiza juhudi za kumaliza uhalifu huo kwani maafisa huwapa tarifa pindi wanapotaka kufanya operesheni na hivyo watu hao kukimbia kutokana na baadhi ya maafisa wa ngazi za juu katika Idara ya Huduma za Polisi kushindwa kukabiliana na magenge hayo.

Aidha ameongeza kuwa, hali hiyo ni chanzo cha kuibuka upya kwa magenge hayo hatari ambayo yamehusika katika visa vya uhalifu vinavyojumuisha kudunga watu visu na wizi wa mabavu.

Guardiola asifia ujio wa meneja mpya Spurs
Ni zamu ya Lilepo, Ngoma Young Africans