Afisa Habari wa Maafande wa Jeshi la Magereza Tanzania Prisons’, Jackson Mwafulango amesema wapo tayari kupambana na kubeba alama tatu mbele ya Namungo FC leo Jumamosi (Machi 11) kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Prisons inashika nafasi ya 14 ikiwa na alama 22 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na imekuwa katika hekaheka za kujinasua kwenye nafasi hiyo iliisalie kwenye ligi hiyo.

Mwafulango amesema baada ya kupoteza mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya mabingwa watetezi, Young Africans kwa mabao 4-1, kikosi chao kilifanyia kazi upungufu kwenye eneo la ushambuliaji ambalo lilikuwa likikosa mabao licha ya kupata nafasi nyingi za kufunga.

“Tumeshawasili huku Lindi kwa ajili ya mchezo wetu wa leo, kocha amekiandaa kikosi vile ipasavyo kilichobaki ni wachezaji kufanya vizuri tu uwanjani. Ninaamini kuanzia mchezo wa leo Jumamosi dhidi ya Namungo FC tunaanza kuhesabu alama tatu hadi mchezo wa mwisho msimu huu,” amesema Mwafulango.

Shomari Kapombe afichua siri nzito
Fidia bonde la Mto Msimbazi: Serikali yatoa ufafanuzi