Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amemsifu mtangulizi wake, Lazaro Nyalandu kwa kazi aliyoifanya na kuahidi kuiendeleza.

Akiongea baada ya makabidhiano ya ofisi, Profesa Maghembe alisema kuwa ataendeleza mambo mazuri ambayo yalifanywa na Nyalandu aliyekuwa waziri wa wizara hiyo.

“Vitu ambavyo umevifanya katika kuhakikisha kwamba misitu yetu inapanuka vizuri. Vitu ambavyo umefanya kuhakikisha kwamba utalii wetu unasonga mbele na mpango wa utangazaji wa utalii umezinduliwa hivi karibuni ni vitu vikubwa sana ambavyo umevifanya. Na umevifanya kwa uzalendo mkubwa sana,” Profesa Maghembe alimwambia Nyalandu.

Awali, baada ya kuapishwa wiki hii Ikulu jijini Dar es Salaam, Profesa Maghembe alitangaza kiama kwa majangili na watu wote wanaohujumu maliasili na utalii wa nchi.

 

Ripoti: Viongozi 10 waandamizi wa ISIS wauawa Syria, Iraq
Serikali Yawaonya Wanaoiadhibu Mifugo