Rais wa Urusi, Vladimir Putin ametangaza kupitia luninga ya nchi hiyo uwepo wa mkutano uliopangwa kufanyika kati yake na Rais wa China, Xi Jinping nchini Uzbekistan wiki ijayo huku akidaiwa kutoa sauti ya dharau.
Mkutano huo, unaweza kuisaidia Kremlin kupanua uhusiano wake na China, nchi ambayo Putin ameiita mshirika “imara na wa kutegemewa” baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Kukatishwa kwa uhusiano wa kiuchumi na nchi za Magharibi, kumeisukuma Urusi katika mwelekeo wa haraka wa uchumi wake kuelekea Asia hasa Uchina, na kufanya mkutano na Xi kuwa wa muhimu sana.
Katika maelezo yake, Putin amesisitiza kuwa nchi za Magharibi zimeshindwa katika “uchokozi wake wa kiuchumi, kifedha na kiteknolojia” dhidi ya Russia.
Ingawa Beijing haijatangaza kuunga mkono uvamizi huo, hata hivyo imerejea hoja za mazungumzo za Kremlin kwamba Marekani ndiyo “mchochezi mkuu” wa mzozo huo.
China, imeipatia Urusi usaidizi wa kiuchumi huku kukiwa na vikwazo vya Magharibi, kama msambazaji wa kila kitu kuanzia magari hadi simu mahiri na kama mnunuzi wa mauzo ya nishati ambayo hayahitajiki tena katika nchi za Magharibi.
Katika hotuba hiyo, Putin alisema, “Wizara ya Ulinzi ya Urusi imekiri mamia ya vifo nchini Ukraine, ingawa jumla hiyo haijasasishwa kwa miezi kadhaa huku Marekani ikikadiria mwezi uliopita kuwa wanajeshi 80,000 wa Urusi walikuwa wameuawa au kujeruhiwa katika vita hivyo.