Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia 2022 ‘Timu ya Taifa ya Qatar’ wameingia kwenye Kashfa ya kupanga matokeo, kufuatia kuhusishwa kutoa Mlungula kwa Wachezaji wa Timu ya Taifa Ecuador, ili kuhakikisha wanapoteza mchezo wa ufunguzi keshokutwa Jumapili (Novemba 20).

Mchezo huo wa ufunguzi utapigwa mjini Al Khor katika Uwanja wa Al Bayt, ambapo kutakuwa na mchezo mmoja tu kabla ya England kumenyana na Iran siku moja baadae.

Taarifa za Kashfa hiyo zimetolewa na Mkurugenzi wa kituo mafunzo na Utafiti cha Uingereza Mashariki ya kati chenye maskani yake Bahrain ambaye pia ni Mwandishi wa kitabu cha ‘The Deception of the Arabs’ Amjad Taha.

Taha ameandika katika ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Twitter akidai Wachezaji 8 wa Ecuador wamehongwa kiasi cha Dola milioni 7.4 na Qatar ili wapoteze mchezo huo kwa tofauti ya 1-0 katika kipindi cha pili.

Taha ameripoti kuwa ingawa anatumai kuwa habari hiyo ni ya uwongo, pia anatumai kwa kushiriki habari hiyo itabadilisha matokeo.

Kitabu cha ‘The Deception of the Arabs’ kinachomilikiwa na Amjad Taha kinaakisi ufahamu wake juu ya masuala ya Mashariki ya kati.

Qatar itashiriki kwa mara ya kwanza Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu 2022 kama mwenyeji, huku Ecuador ikishiriki Fainali hizo kwa mara ya pili.

Kwa mara ya kwanza Ecuador ilishiriki Fainali hizo mwaka 2002 zilizofanyika Korea Kusini na Japan, na mwaka 2006 zilizounguruma nchini Ujerumani.

Wapiga kura kupata mpatanishi wa Kitaifa
Washindwa kuchagua Rais kwa mara ya sita