Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli leo ametoa msamaha kwa mwanamuziki maarufu Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Jonson Nguza maarufu kama Papii Kocha waliokuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela.

Msamaha huo pia umewagusa wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa, akiagiza wote waachiwe kati ya leo na kesho.

Aidha, kwa ujumla Rais ametoa msamaha kwa wafungwa 8157 na kuagiza kati yao 1828 waachiwe leo huku wengine 6329 watapunguziwa muda wa kukaa gerezani.

Msamaha huo umetolewa leo katika siku ya maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara, ambapo ametumia ibara ya 45 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayompa mamlaka ya kutoa msamaha huo.

Akitoa sababu za kutoa msamaha kwa waliotumikia kifungo cha maisha au kunyongwa, alisema walifuatiliwa na kubainika kuwa ni kweli wamekuwa wakiishi maisha ya ‘wokovu’ huku wengine wakiwa na umri mkubwa wakitumikia ujana wao wote ndani ya magereza.

 

 

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 10, 2017
Israel yaifyatulia Palestina Makombora