Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amehutubia viongozi, Makatibu Mahsusi pamoja na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka kabla ya kufunga Mkutano wa Kitaaluma wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) pamoja na Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) uliofanyika Fumba Zanzibar, Mei 27, 2023.

Akiongea katika Mkutano huo, Rais Samia amewataka watunza kumbukumbu na nyaraka TRAMPA, na makatibu mahsusi – TAPSEA, kuzingatia kiapo cha uaminifu katika kutunza siri kwa kuwa kina maana kubwa katika utendaji wa kazi zao.

Amesema, “ufanisi maana yake ni kuikamilisha kazi vile inavyotakiwa, kwa kiwango kinachotakiwa na wakati unaotakiwa. Ukiwa na nidhamu na uadilifu utazalisha kazi kwa wakati kwa kiwango kinachotakiwa na muda unaotakiwa,”

Aidha ameongeza kuwa, kiapo cha uaminifu cha kutunza siri walichokula mbele ya Wakili Mkuu wa Serikali na yeye kushuhudia wakizingatie kwa kuwa kina maana katika utendaji kazi wao wa kila siku na kusema, “sasa kati yenu mtu akienda kinyume na kiapo chake alichokula akishuhudiwa na Rais wa nchi, tutajuana huko mbele kwa mbele, kwa hiyo naomba muishi kiapo chenu.”

Pia Rais Samia amesema ni muhimu kwa waajiri na wakuu wa taasisi katika sekta ya umma na sekta binafsi kuwaruhusu watunza kumbukumbu na nyaraka na makatibu mahsusi kushiriki mafunzo ya uadilifu na utunzaji siri, ili kuwajengea uwezo na ufanisi katika kazi zao.

Zifuatazo ni picha zikionesha baadhi ya matukio wakati wa kikao hicho.

Nasreddine Nabi afunguka mbinu za USM Alger
Wanachama SADC washirikiane utatuzi wa changamoto