Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein ametoa msamaha kwa wafungwa 19 ambao bado walikuwa wakiendelea kutumikia vifungo magereza ya Unguja na Pemba, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 56 ya mapinduzi ya Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na katibu wa balaza la mapinduzi na katibu mkuu kiongozi, Dkt. Abdukhamid Yahaya Mzee, imeeleza kuwa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 59 cha katiba ya Zanzibar 1984, Rais Shein ameamuru kuwa kifungo kilicho baki cha wafungwa wote waliopata msamaha kifutwe na waachiwe huru.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Zanzibar inasherehekea miaka 56 ya mapinduzi na Rais ameridhika kwakuwa kuna sababu za kutosha kutumia uwezo wake huo katika sherehe hii kuachia wafungwa hao.

Msamaha huo ambao hutolewa kila mwaka katika kipindi cha sherehe za mapinduzi, huwahusisha wafungwa ambao ni wazee sana, wenye maradhi sugu au wenye makosa madogo ambao wamebakiza muda mfupi wa kutumikia kifungo sambamba na kuonesha nidhamu nzuri.

Tabia 10 za wanaume zisizopendwa na wanawake
Video: Bosi Nida anavyopitia katika tanuru la moto

Comments

comments